Tuesday 1 November 2016

WANAWAKE WAKIAFRIKA WANAVYOPENDEZA NA MITINDO MBALIMBALI YA NYWELE

 misuko mbalimbali ya nywele kwa wakina dada na kina mama inaonekana kuwapendeza sana lakini watu husema kupendeza kwa msuko wa nywele kuna tokana na sura ya mtu inaonekana kuwa kweli kama tunavyomuona mwana dada hapo juu ametengeneza nywele yake inayojulikana kwa jina la dredi lakini pia ameutengeneza mtindo wa nywele hiyo na amependeza sana.
 mwanadada hapo juu ametengeneza msuko unaojulikana kwa jina la crochet ni msuko ulioingia sana kwa sasa na mara nyingi hupenda kuutumia kwa wakina dada lakini pia unawapendeza sana wahenga husema kizuri kipewe sifa.

mwanamke urembo dada anaonekana kutoa tabasamu zuuri la furaha kama tunavyomuona na msuko wake mzuri kabisa anaonekana kuvutia zaidi nywele ni kitu bora kwa wanawake.

MITINDO YA VITENGE KWA WANAWAKE

 vazi la kitenge limeonekana kupamba moto hadi kufikia hatua ya wageni kutoka katika nchi za kigeni kupendezewa na vazi hilo hadi kuamua kuliweka kwenye fasheni ya sasa hivi,sio wazungu pekee ambao wametokea kuvutiwa na vazi hilo kwani hata waafrika wenyewe hupendezwa na vazi hilo.

hata hivyo vazi hili la kitenge huwapendeza wanawake wengi lakini pia linaonekana ni vazi la heshima kwa wakina mama tunaona hata wake wa marais barani Afrika huvaa vazi hilo na kupendeza sana.
 aidha wakina dada nao hawako nyuma sana na kivazi hichi cha vitenge kwani husema kitenge ndo habari ya mjini saivi,hushona mishono mbalimbali waitakayo na mishono hiyo inaonekana kuwafanya wakina dada hao kuvutia zaidi.
kitenge ni vazi unaloweza kuvaa kila sehenu kama maofisini,mikutanoni kwa wale wanafunzi wa vyuo wanaojua mitindo hapa ndo pahaliake lakini pia unaweza ukashona kikoti au blauzi nzuri inayofaa kuvalia suruali na kuonekana maridadi kabisa.usibaki nyuma mwanamama kina dada kitenge ndio habari ya mjini.

FLAVIANA MATATA AFUNGUKA JUU YA FOUNDATION ALIYOANZIA.

Mwanamitindo wa TZ ambaye yuko kwenye HEADLINES za Kimataifa.. Nimekutana na kitu kinachomuhusu yeye mtandaoni, nikaona kwa sababu ni mtu wetu basi niisogeze hii ili watu wake pia waone.
Kaingia kwenye HEADLINES za Magazine kubwa duniani, BLACK ENTERTAINMENT ambao wamefanya nae exclusive interview, mengi kayasema hapa mengine hata sikuwahi kuyajua kutoka kwake.. kumbe ishu ya kuingia kushiriki Miss Universe hata hakuwa na idea ya kitu anachokifanya, aliingia kwa kujifurahisha tu !!
Kingine alichokiongea ni ishu ya Flaviana Matata Foundation, taasisi ambayo aliianzisha kwa ajili ya kusaidia wasichana yatima kwenye masuala mbalimbali ikiwemo mahitaji muhimu ya Shule.
Niliwahi kumuona marehemu mama yangu akisaidia watoto wengine kuwapeleka shule.. Nilikuwa mdogo sana lakini alikuwa akituambia na ndugu zangu umuhimu wa kusaidia watu ambao wanahitaji msaada.. Nilianzisha FMF kwa ajili ya moyo wa kujitolea..Flaviana Matata.
Jitihada nnazozifanya kusaidia wasichana kupata elimu itakuwa ni kitu ambacho kila mtu anaweza kukipongeza..– Flaviana Matata.
Safari ya staa wetu wa mitindo inaendelea yani, kwenye exclusive hiyo amesema moja ya changamoto iliyopo TZ ni watu wachache kutoa support kwenye misaada anayotooa kwa kuwa ni wachache ambao wanajua maana ya kujitolea kwa jamii.