Mwanamitindo
wa TZ ambaye yuko kwenye HEADLINES za Kimataifa.. Nimekutana na kitu
kinachomuhusu yeye mtandaoni, nikaona kwa sababu ni mtu wetu basi
niisogeze hii ili watu wake pia waone.
Kaingia kwenye HEADLINES za Magazine kubwa duniani, BLACK ENTERTAINMENT ambao
wamefanya nae exclusive interview, mengi kayasema hapa mengine hata
sikuwahi kuyajua kutoka kwake.. kumbe ishu ya kuingia kushiriki Miss Universe hata hakuwa na idea ya kitu anachokifanya, aliingia kwa kujifurahisha tu !!
Kingine alichokiongea ni ishu ya Flaviana Matata Foundation, taasisi ambayo aliianzisha kwa ajili ya kusaidia wasichana yatima kwenye masuala mbalimbali ikiwemo mahitaji muhimu ya Shule.
“Niliwahi
kumuona marehemu mama yangu akisaidia watoto wengine kuwapeleka shule..
Nilikuwa mdogo sana lakini alikuwa akituambia na ndugu zangu umuhimu wa
kusaidia watu ambao wanahitaji msaada.. Nilianzisha FMF kwa ajili ya
moyo wa kujitolea..“–Flaviana Matata.
“Jitihada nnazozifanya kusaidia wasichana kupata elimu itakuwa ni kitu ambacho kila mtu anaweza kukipongeza..“– Flaviana Matata.
Safari
ya staa wetu wa mitindo inaendelea yani, kwenye exclusive hiyo amesema
moja ya changamoto iliyopo TZ ni watu wachache kutoa support kwenye
misaada anayotooa kwa kuwa ni wachache ambao wanajua maana ya kujitolea
kwa jamii.
No comments:
Post a Comment