vazi la kitenge limeonekana kupamba moto hadi kufikia hatua ya wageni kutoka katika nchi za kigeni kupendezewa na vazi hilo hadi kuamua kuliweka kwenye fasheni ya sasa hivi,sio wazungu pekee ambao wametokea kuvutiwa na vazi hilo kwani hata waafrika wenyewe hupendezwa na vazi hilo.
hata hivyo vazi hili la kitenge huwapendeza wanawake wengi lakini pia linaonekana ni vazi la heshima kwa wakina mama tunaona hata wake wa marais barani Afrika huvaa vazi hilo na kupendeza sana.
aidha wakina dada nao hawako nyuma sana na kivazi hichi cha vitenge kwani husema kitenge ndo habari ya mjini saivi,hushona mishono mbalimbali waitakayo na mishono hiyo inaonekana kuwafanya wakina dada hao kuvutia zaidi.
kitenge ni vazi unaloweza kuvaa kila sehenu kama maofisini,mikutanoni kwa wale wanafunzi wa vyuo wanaojua mitindo hapa ndo pahaliake lakini pia unaweza ukashona kikoti au blauzi nzuri inayofaa kuvalia suruali na kuonekana maridadi kabisa.usibaki nyuma mwanamama kina dada kitenge ndio habari ya mjini.
No comments:
Post a Comment